Monday 27 May 2013

VIJANA WANATEMBEA TANZANIA




  1. Maandalizi ya eneo la maonyesho ya kila mwaka ya Utalii ya Karibu yameanza kushika hatamu kwenye viwanja vya Magereza, nje kidogo ya jiji la Arusha. Maonyesho hayo ambayo yataanza rasmi tarehe 31 Mei 2013 yanatarajiwa kuwaweka pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii toka ndani na nje ya nchi kwa muda wa siku tatu. Post hii inakuletea picha kadhaa zikionyesha maandalizi ya awali ya mabanda ya maonesho yakiwa yanaendelea kwenye viwanja vya Magereza.


    Msimamizi wa eneo la Maonesho Bw. Hassan (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa waratibu wa maonesho haya Bw. Sam Diah(kulia)
    Acting CEO wa TATOTZ Bw Cyril (kulia) akiteta jambo na Mratibu wa Karibu Fair 2013

    Wamama na wadada hawapo nyuma, nao wapo ulingoni kuweka sawa mambo kwa ajili ya maandalizi ya Karibu fair 2013. Picha zote kwa hisani ya mdau Sam Diah wa Arusha
    0

    Add a comment



  2. 0

    Add a comment



  3. Horombo

    Horombo

    Horombo

    Horombo

    Horombo

    Horombo
    0

    Add a comment



  4. Ni Taswira zilizopigwa Mwezi Januari Mwishoni mwaka huu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. Unapokuwa umelala ndani ya Hifadhi unakuwa na fursa ya kuweza kuanza matembezi mapema kidogo tofauti na yule aliyelala nje ya Hifadhi ambae atalazimika kusubiri hadi pale ambapo geti la hifadhi litakapofunguliwa na kumruhusu.

    0

    Add a comment



  5.  Ni Taswira ambazo Mdau Jumaa wa River Spring  (Lushoto) amezitupia kwenye wall yake ya Facebook zikionyesha maeneo kadhaa ya mji wa Singida na baadhi ya mambo ambayo wengine hatuyajui kuhusu Singida. Mdau Jumaa alikuwa huko siku kadhaa na hapo juu ni picha aliyoipiga mida ya jioni akiwa pembezoni ya Ziwa Singida ambalo lipo mkoani hapo. Picha hii ilipigwa mida ya jioni na Ziwa likionekana kwa Nyuma.

    Ziwa Singida Likionekana kwa mbali



    Mitaa ya kati ndani ya Singida Mjini



    tembelea FB page ya River Sping ConneXions "Lushoto" 
    au Blog ya Amazing Lushoto
    upate kujua mengi kuhusu project hii ya mdau Jumaa
    0

    Add a comment



  6. Moja ya jambo ambalo inakubidi ujiandae kiakili ni kuwa na ujasiri wa kukaa siku zote za safari yako bila kuoga. Ukweli ni kwamba hali ya hewa ya huku hairuhusu hata mtu kufikiria kutoa nguo na kuanza kujimwagia maji. Aidha yatakuwa ya moto sana na mwishowe yakuletee madhara ya joto, au yatakuwa yabaridi yakuletee madhara ya baridi. Unaweza kubahatisha kwa maeneo ya Mandara lakini ukiingia anga za Horombo kwenda mbele basi sahau kabisa. Haimaanishi zoezi zima la usafi wa mwili linawekwa kiporo, la hasha! Kila siku kunapokucha unaletewa bakuli yenye maji ya uvuguvugu kama zinavyoonekana kwenye  picha ya juu. Hapo kila mmoja ana bakuli ya kwake. Wewe mgeni ndio unakuwa na uhuru wa ni namna gani unaweza kuyatua maji hayo kusafishia mwili. Kwa wengi maji huwa ya kunawia uso au kunawia sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia kitaulo kidogo. Kwa usafi wa kinywa unaletewa maji kwenye chupa yako ya kunywea kwa ajili ya kupigia mswaki. Vyumba vya mabafu vipo sambamba na maliwato lakini sidhani kama utamuona mtu akiingia na ndoo ya kuogea huko.

    Mdau  akiendelea na usafi asubuhi moja kwenye banda letu tulipokuwa katika kituo cha Horombo
    0

    Add a comment



  7. Saadani National Park - where nature and beach meet
    Hii ni combo ambayo ina vyumba vinne, kila kimoja self contained pamoja na Sebule moja ambayo ni shared (inayoonekana pichani). Kuna kuwa na jiko ambapo kama mgeni ataamua kujipikia mwenyewe (au aje na mpishi wake) basi nae anakuwa na ofisi yake. Luninga hapo ni full DSTV
    Saadani National Park - where nature and beach meet
    Mdau Abdul Kimanga wa Sherehe yetu Blog alikuwa huko kwa Vakesheni yake mwezi Desemba mwaka jana. Wasiliana na tour operator wako au aliye karibu nawe ili akupe mpango mzima wa kufika na kufurahia mandhari ya Saadani. Kwa Mdau uliye Dar, Saadani ndio Hifadhi iliyo karibu kabisa na jiji la Dar kwa kupitia njia ya Bagamoyo.
    0

    Add a comment



  8. Sio njia zote za kupandia mlima Kilimanjaro ambazo mgeni hushukia pale alipoanzia, Zipo baadhi ambazo mgeni hushukia njia nyingine. Rongai, Umbwe ni njia ambazo zina utaratibu huu. Wa Umbwe hushukia njia ya Mweka wakati wale wa njia ya Rongai hushukia njia ya Marangu. Kwa kuwa Mabanda ya njia ya Marangu ni kwa ajili ya wale wanaoitumia njia ya Marangu, wanaotoka Rongai wao hulala kwenye mahema walioanza nayo safari. Hapa ni kituo cha Mandara na haya mahema ni ya wapandaji wa Mlima Kilimanjaro walioanzia safari yao kwenye geti la Rongai na hapa (Horombo) wakiwa njiani kurudi chini kupitia njia ya Marangu.
    Horombo Hut - Marangu route
    Hapo kuna mahema ya Kulala (madogo) na kuna mahema ya Mesi (chakula). Wapishi na wagumu wao nao wanalala kwenye mahema yao.

    Horombo Hut - Marangu route
    Hili lilikuwa kundi jingine likiwa limeshajenga kambi yao.

    Horombo Hut - Marangu route
    Vifaa vyao vyote hubebwa na Wagumu wao wakiwa safarini.

    Horombo Hut - Marangu route
    Siku hii Ukungu na baridi vilishika hatamu si mchezo. Sisi tuliokuwa tunalala kwenye mabanda tuliisikia baridi kisawasawa. Sijui hawa ndugu zetu waliolala kwenye haya mahema walikuwa na hali gani usiku mnene ulipotinga. Aina ya malazi unayoyapata ukiwa unapanda mlima Kilimanjaro iwe ni kigezo cha msingi kwenye uchaguzi wa njia ya kupandia Mlima huu.
    0

    Add a comment



  9. Hili lilikuwa ni kundi la wanafunzi wa shule moja tokea Arusha ambao nao walikuwa wanapanda mlima Kilimanjaro. Tulianza nao kupanda Mlima siku moja kwa njia ya Marangu lakini wao walikuwa na mpango tofauti kidogo na tuliokuwa nao sisi. Sisi tulipanga kukaa kituo cha Horombo kwa siku mbili ili mwili uweze kuzoea mazingira ya juu, hawa wanafunzi wao walikuwa na mpango wa kwenda kufanya acclimatisation kwenye kituo cha Kibo. Hivyo tulipofika Horombo, siku iliyofuata wao waliondoka kuelekea Kibo na kutuacha sisi kituo cha Horombo tukifanya acclimatisation kwa kwenda Zebra rock na siku iliyofuatia kuendelea na safari yetu kwenda Kibo. Kusema ukweli, mpango wao ulikuwa mzuri na faida kwao kwani asilimia kubwa ya hawa wanafunzi hawa waliweza kufika kilele cha Uhuru. 
    Kundi hili lilinikumbusha mbali kidogo, lilinikumbusha kipindi nasoma sekondari ambapo shuleni kulikuwa na utaratibu wa kwenda kupanda mlima Kilimanjaro wakati wa zile likizo fupi za wiki moja mwezi wa tisa. Mara kadhaa nilijaribu kuomba ruhusa na ufadhili kwa wazazi lakini mara zote maombi yangu yaligonga ukuta kwa sababu kadha wa kadha. 
    Picha juu ni wanafunzi hao wakipiga picha ya pamoja kwenye kituo cha Horombo kabla hawajaondoka kuelekea kituo cha Kibo.
    0

    Add a comment



  10.  Ni Kipita shoto maarufu ndani ya jiji la Mwanza kijulikanacho kama Sanamu ya Samaki. Hapo siku za sikukuu huwa panajaa watu ambao huenda kupumzika huku wengi wakiwa na nia ya kupiga picha na sanamu ya Samaki iliyopo kwenye kipita shoto hiki. Picha hii niliipiga siku ya sikukuu ya Pasaka mwaka huu (2013).


    0

    Add a comment

Loading

No comments:

Post a Comment