Maandalizi ya eneo la maonyesho ya kila mwaka ya Utalii ya Karibu
yameanza kushika hatamu kwenye viwanja vya Magereza, nje kidogo ya jiji
la Arusha. Maonyesho hayo ambayo yataanza rasmi tarehe 31 Mei 2013
yanatarajiwa kuwaweka pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii toka
ndani na nje ya nchi kwa muda wa siku tatu. Post hii inakuletea picha
kadhaa zikionyesha maandalizi ya awali ya mabanda ya maonesho yakiwa
yanaendelea kwenye viwanja vya Magereza.
Msimamizi wa eneo la Maonesho Bw. Hassan (kushoto) akibadilishana mawazo
na mmoja wa waratibu wa maonesho haya Bw. Sam Diah(kulia)
Acting CEO wa TATOTZ Bw Cyril (kulia) akiteta jambo na Mratibu wa Karibu Fair 2013
Wamama na wadada hawapo nyuma, nao wapo ulingoni kuweka sawa mambo kwa
ajili ya maandalizi ya Karibu fair 2013. Picha zote kwa hisani ya mdau
Sam Diah wa Arusha
Add a comment