Kitaifa
Jeshi lafanikiwa kudhibiti vurugu Mtwara
Posted Mei25 2013 saa 20:33 PM
Kwa ufupi
Hatimaye Soko Kuu la Mjini Mtwara limefunguliwa
baada ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kutwaa jukumu la kulilinda
ili wananchi wapate huduma muhimu za chakula.
Mtwara. Mkuu wa vikosi vya aridhini wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali SM Kijuu amewahakikishia
ulinzi wafanyabiashara hao, baada ya kukutana na uongozi wa Chama cha
Wafanyabiashara Sokoni (Wabisoco) jana asubuhi, kufuatia wafanyabishara
hao kudai kuendelea kusitisha biashara zao kwa kuhofia usalama.
Katibu wa Wabisoco, Saidi Namata ameliambia
Mwananchi Jumapili kuwa wafanyabiashara hao wamekubaliana kufungua
biashara zao, baada ya makubaliano ya kulinda eneo hilo na askari wa
JWTZ.
“Sisi wafanyabiashara tulikuwa tayari kuendelea
kusitisha huduma kutokana na hali ya usalama kuwa mbaya, alipokuja
kiongozi wa jeshi na kutuhakikishia kuwa dhamana ya ulinzi itakuwa chini
yao tulikubaliana,” alisema Namata
Alisisitiza: “Kama ulinzi ungekuwa mikononi mwa
polisi, katu tusingefungua. Polisi wenyewe ndiyo hawa wanaovunja maduka
na kuiba, kwa kuwa dhamana hii imebebwa na wanajeshi hatuna shaka,
tunaomba wafanyabiashara wengine wafungue biashara zao.”
Tangu juzi magari ya matangazo yamekuwa yakipita
mjini Mtwara na kuwatangazia wananchi kuendelea na kazi zao kama kawaida
kwa kuwa ulinzi umeimarika, huku askari wa JKT na JWTZ waliosheheni
silaha wakizunguka mitaani.
Pinda awasili Mtwara
Wakati tukiewnda mitamboni Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewasili Mtwara jana jioni na kukutana na viongozi wa mkoa.
Bungeni Dodoma
Suala la mgawanyo wa rasilimali za taifa jana
liliendelea kutikisa Bunge, baada ya baadhi yao kueleza kuwa ni haki kwa
maeneo yanakotoka rasilimali hizo kunufaika kwanza kabla ya maeneo
mengine.
Wakati wabunge hao wakieleza hayo, wengine
wamesisitiza kuwa kwa kuwa nchi ni moja Tanzania, rasilimali zote ni
mali ya Watanzania wote.
Wabunge wanaotaka rasilimali zinufaishe kwanza
maeneo zinakotoka. Wanasema pamoja na ukweli kwamba Tanzania ni moja,
watu hao wana haki ya msingi kupata huduma hizo kwanza kuliko wengine.
Mbunge wa Msalala (CCM), Ezekiel Maige alisema
anashangaa kwa nini fomula ya rasilimali kuyaendeleza maeneo
iliyopatikana, inatumika kwenye Idara ya Wanyamapori na haitumiki katika
sekta ya nishati na madini.
- Vurugu hizi za Mtwara zitoshe kuwa fundisho, somo kwetu
- Faini juu, ajali bado zinaongezeka
- Kutana na mashuhuda wa bomu lililoua Arusha
- Hukumu kesi ya uporaji wa Sh239 mil za NMB sasa kutolewa Juni 4
- ‘Acheni maandamano ya kijinga’
- Kesi ya Richmond kufufuliwa
- ‘Mgogoro wa Fahari wawili’ waendelea
- Watu wengine 10 wakamatwa Iringa
- Usajili: Wafahamu wachezaji waliopo sokoni
- Umuhimu wa viwanja vya michezo unasahaulika
- Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka
- Sitta ataja wanaotetea nchi
- Jeshi lafanikiwa kudhibiti vurugu Mtwara
- Lema amvaa Lowassa kwa helikopta Monduli
- Upo uwezekano wa kupata rais mwanamke, 2015?
- Wawekezaji 45 kuwekeza Mtwara
- Wizara ya Elimu yapangua ratiba rasmi ya Bunge
- JWTZ wakanusha taarifa za askari kujihusisha na makahaba DRC
- Usajili: Wafahamu wachezaji waliopo sokoni
- Kagera: Simba wametuliza
No comments:
Post a Comment