Monday 27 May 2013

Mashuhuda wa bomu lililotupwa kanisani ;walishuhudia lilivyotua chini mpaka linalipuka


Habari Ya Ndani

Mashuhuda wa bomu lililotupwa kanisani ;walishuhudia lilivyotua chini mpaka linalipuka

Share bookmark Print Email Rating
Fatuma Tarimo akionyesha kipande cha chuma kilichotolewa kwenye mguu wake. Picha na Maktaba 
Na Freddy Azzah, Mwananchi  (email the author)

Posted  Jumatatu,Mei27  2013  saa 12:41 PM
Kwa ufupi
  • Kwa wakati huo, hata maumivu nilikuwa siyasikii, nikataka kukimbia, ardhi siioni, ninaona tu kama napelekwa huku na huku, nikasema nitashindana na hizi nguvu mpaka saa ngapi, nikasema ngoja nitulie.
SHARE THIS STORY
0
Share


Mei 5 mwaka 2013 ni siku ambayo haitafutika katika historia ya Tanzania kutokana na tukio la kusikitisha la kutupwa kwa bomu kanisani, ambapo watu watatu walifariki na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
Tukio hilo lilitokea mbele ya Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Askofu Mkuu Francisco Montecillo, Askofu Mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha, walipokuwa wakizindua jengo la Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Arusha.
Siku hiyo iliyoleta historia mbaya kwa taifa letu kutokana na tukio hilo ambalo viongozi mbalimbali waliliita la kigaidi, halitaweza kusahaulika kwa baadhi ya watu ambao wanasimulia:
Fatma Tarimo (39), mkazi Olasiti mkoani Arusha. Yeye, ambaye ni mama wa watoto watano, anasema siku ya tukio aliamka asubuhi akiwa ni mtu mwenye furaha kuliko siku zote huku akiwa shauku ya kumaliza shughuli zake mapema kisha awahi kanisani.
Anasema kuwa kabla ya kujiandaa kwenda kanisani aliwatayarisha watoto wake ili watangulie.
Mama huyo ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Burka Estate, anasema baada ya watoto wake kuondoka yeye alibaki nyumbani ili kumtayarishia chakula mama yake aliyekuwa amemtembelea.
Anaeleza kuwa, baada ya kumaliza shughuli zake alijiandaa na kwenda kanisani ambapo alipata lifti ya gari la watawa wa kanisa hilo.
“Pale kuna misa mbili, siku nyingine watoto huwa wanakwenda misa ya pili, lakini siku ile kwa sababu ya ufunguzi wa jengo la kanisa kulikuwa na misa moja, mimi nikasema watoto watangulie kanisani na mimi nimtayarishie kwanza mama chakula,” anasema.
Anasema kuwa, walipofika kanisani walikaa nyuma huku mbele kukiwa na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo, watawa, pamoja na vikundi mbalimbali vya kwaya.
Aeleza bomu lilivyolipuka
Bomu lile halikutua mbali sana na nilipokuwa, ilikuwa kama umbali wa hatua moja tu na lilipotua chini watu walisogea pembeni kidogo na eneo lile kulikuwa na watoto wengi.
Nakumbuka wakati huo misa ilikuwa inaendelea na viongozi walikuwa wamesimama tayari kwa kuzindua jengo, niliona kitu kama chuma kimerushwa kikatua pembeni mwangu.
1 | 2 | 3 Next Page»

No comments:

Post a Comment